busara ya maisha

~David Kiriinya

Nimeshindwa kuyakinga, yanonisuta kutoka
Moyoni yametanda, kama makubwa majoka
Kuchao ni mawazo, ya maisha yalonitoka
Nitembeapo nachomwa, na jua la mchana
Nikitafuta chakula, kwa marefu na mapana
Kila mara nawasikia wakinikejeli eti kijana

Ewe mola nijalie, nitabasamu usoni 

Migodini kwa hamu nachimba, huku misuli nikiinyosha
Bosi wangu yuanisuta, matusi akiyaporomosha
Mgongo nimeupinda, na mikono nayo kukausha
Shuleni niliwaaga, wenzangu masomoni
Chuo kikuu gharama, nisiyoiweza mimi masikini
Nilitamani Uhandisi, lakini sina hata sumni

Ewe Mola nijalie, nitabasamu usoni 

Matembezi kijijini, ni mapenzi ya askari
‘Tupe chetu twende, au tuseme ulilewa chakari’
Pato langu nawapa, la kununua sukari
Alfajiri korokoroni, mwanao katiwa mbaroni
Madai ya uwongo si haba, eti kambaka Cheroni
Masikini kweli hana chake, hata senti za jandoni

Ewe Mola nijalie, nitabasamu usoni

Naishi kwa matumaini, ya mazuri maisha
Nikikumbuka adabu na heshima, ajuza barabarani kumpisha
Nitapata visenti mwakani, kula vyema na pia kujivisha
Nawasihi wenzangu, utu wema hauna gharama
Kwani binadamu ni maua, sote twaingoja ya kiama
Ukimwona usimpite, masikini aliyeshika tama

Ewe Mola tujalie, tutabasamu usoni

Advertisements

comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s